Mkuu Wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania Upendo Richard(Katikati) akishirikiana na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom Kinondoni Donart Alwatani kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa huduma kwenye duka hilo jipya lililopo eneo la Kinondoni Manyanya Dar es salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Duka hilo litakuwa likitoa huduma kwa siku saba za wiki ikiwemo siku za sikukuu.
Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Tanzania,Bi.Upendo Richard (wa pili kushoto) akiwawekea Shampeni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa tatu kushoto) na Msimamizi wa Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanaya Jijini Dar es salaam Donard Alwatani ikiwa ni ishara ya kulitakia mafanikio duka hilo mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Anaeshuhudia ni Meneja Uhusiano kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(katikati) akiwa kwenye furaha baada ya kufungua Shampeni kuashiria kuanza rasmi kwa huduma katika duka jipya la kampuni yake lilipo Kinondoni Manyanya Dar es salaam. Kutoka kulia ni Msimamizi wa duka hilo Donart Alwatani, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim, Mkuu wa Idara ya Mauzo ya rejareja wa Vodacom Upendo Richard na Meneja katika idara hiyo Elihuruma Ngowi.
Hili ndilo Duka jipya la Vodacom lililopo Kinondoni Manyanaya Jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...