Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (kushuto )  pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Mh. Anthony Mtaka wakati alipotembelea sehemu iliyoathirika kwa mafuriko,Mkoani Morogoro.
Muonekani wa Dajara lilillokatika kutokana na Mafuriko yaliyotokea hivi karibuni.
Musururu wa malori yaliyo kwama baada ya mafuriko yaliyotokea mkoani Morogori hivi karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mkandarasi gani alijenga hilo daraja?Anastahili "KUDOS".Daraja imara sana hilo kuweza kustahimili huo 'muziki'.Blog ya jamii asante kwa hizo picha za hewani(Aerial photos) walau wengi tumeelewa kilichotea.

    David v

    ReplyDelete
  2. MAFURIKO HAYA YANATOKANA NA UHARIBIFU WA MISITU ILIYOKO KWENYE MILIMA WILAYANI MVOMERO. MIAKA KUMI NA TANO VILIMA VYA MVOMERO VILIKUWA NA MITI MITI MINGI LAKINI WACHOMA MKAA WAKACHIWA WAIKATE MITI HIYO AMBAPO HIVI SASA HATA MVUA KIDOGO TU IKINYINYESHA MAJI HUPOROMOKA KWA KASI KUBWA SANA YAKISOMBA MAWE, MAGOGO NA UDONGO, HIKI NDICHO TUNACHOSHUHUDIA HIVI SASA NA BILA KUZUIA HALI HII BASI MAAFA YATAENDELEA KUTOKEA.

    ReplyDelete
  3. very nice view...kweli mjenga Daraja anastahili pongezi

    ReplyDelete
  4. This is Climate Change REVERSE ACTION!

    Let us learn more to avoid environment destruction and try hard to adapt measures to adapt Climate Change and Mitigation.

    This tragedy give us big lessons!!!

    ReplyDelete
  5. Nakuunga mkono Anonymous wa pili, sababu tatizo kubwa la watanzania tunaangalia sana njaa ya leo, lakini hatuangalii nini kitakachotokea kesho na kuendelea. Wachoma mkaa wanaganga njaa kwa sasa lakini matokeo yake athari zake ni kubwa sana kwa kuharibu mazingira, mafuriko kama haya yalivyo hivi sasa na mengi mengine yataonekanaka. Kesho hao hao wataanza kulia na serikali! serikali!. Imefika wakati watanzania inabidi tubadilike, rasilimali zetu sio tu madini na wanyama, bali kutunza mazingira yetu, ukataji miti hovyo, kulima juu ya vilele vya milima, kulisha hovyo mifugo, imefika mahali wafugaji wawe na ‘zoo’, yaani mfugani awe na eneo ambalo limezungushiwa ambalo atalitunza yeye mwenyewe, na kulisha ng'ombe, mbuzi n.k. bila kuathiri maeneo mengine n.k.Hii tabia ya wafugaji kuhama hama ndio inayoleta migogoro ya ardhi. Pia kupeleka mifugo na kukata miti kwenye vyanzo vya maji ni hatari ya ukame kwa sbb mvua hazitanjesha na zikinyesha ndio mafuriko kama haya kwa sababu hakuna kizuizi. Jamani tuyalinde na kuyahifadhi mazingira yetu, kesho tutakimbilia wapi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...