Wiki mbili tu kuanzia sasa, kitabu changu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences kitatimiza miaka tisa tangu kichapishwe.
Sitaiacha siku hiyo ipite hivi hivi. Nawazia nini cha kufanya. Labda nitaandika ripoti kadhaa juu ya mafanikio yake. Kitabu hiki sikukiandika kwa ajili ya kujipatia pesa, ingawa kimeniletea pesa, tena sio chache.
Lengo langu na mafanikio yangu makubwa yamekuwa katika kuwagusa na kuwasaidia watu. Katika hilo najivunia kazi ngumu niliyofanya katika utafiti na uandishi wake.
Wako wachache ambao wamekuwa wakiniletea kejeli. Hao nawaona kama watu wasio na akili timamu. Kinachoudhi ni kuwa watu hao wanaongelea kitabu ambacho hawajakisoma.
Sitaweza kuleta maoni ya wote waliokisoma wakanipa maoni yao. Hao ni watu makini. Nawashukuru.
Profesa mimi nipo Sweden, nilitamani nipate nakala ya hiki kitabu ili niweze kusoma kilichomo..naweza kipataje???
ReplyDeleteUtoe edition nyingine kama kuna mengine yaliyojitokeza.
ReplyDelete