
Mshindi wa tuzo za mitindo na mbunifu aliyetamba na mavazi ya single button kwa takribani miaka miwili sasa Martin Kadinda anategemea kuanza ziara ya kuonyesha mavazi yake katika nchi kadhaa za kiafrica.
Kadinda amesema kuwa kwa mwaka huu amepanga kufanya maonesho yake nje ya nchi kwa sana kwa kuwa huko ndio kunaitangaza nchi na brand yake kwa ujumla.
Show yake ya kwanza kwa mwaka huu itakuwa Nchini Kenya katika Jiji la Nairobi usiku wa tarehe moja akiwa na wabunifu kutoka tanzania na nchi nyingine za africa Katika Swahili fashion week Kenya... baada ya Kenya safari itakuwa ni Lusaka Zambia ambapo huko atakwenda kuonesha mavazi yake mapya mwishoni mwa mwezi wa tano.
Akizungumzia nguo atakazozionesha Kadinda anasema Supremacy ni mavazi mchanganyiko ikiwepo African shirt ambazo anaziita kwachukwachu kama anavyoonekana pichani.. pia suti zenye vitambaa vya linen and hazitakuwa na solid colour kama ilivyokuwa kwa single button.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...