Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi akimkabidhi hundi ya sh. milioni 2 Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali ya Taifa Muhimbili, Beatrice Mugula kwa ajili ya wagonjwa wa saratani watoto waliolazwa katika hospitali hiyo. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB, Noves Moses. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Mystica Ngongi (wa pili kushoto) akimkabidhi sehemu ya msaada wa nguo, madaftari, sabuni, vitabu vya watoto, Meneja wa jengo la watoto katika hospitali ya Muhimbili, Praxeda Chenya kwa ajili ya kusoma vikiwa na thamani ya sh. milioni moja, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya Muungano. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mahusiano Mwandamizi TPB, Noves Moses na wa pili kulia ni Mkuu wa Idara ya Ustawi ya Jamii Hospitali ya Taifa Muhimbili, Beatrice Mugula. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
 
Wafanyakazi wa TPB wakiweka sawa zwadi kabla ya kuzikabidhi.

 Wafanyakazi wa Benki ya Posta na watoto waliolazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...