Pichani Kulia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd,Alex Msama alipokuwa akizungumza na Wanahabari hivi karibuni kuhusiana na muendelezo wa tamasha la Pasaka 2014.

MAASKOFU wa Makanisa mbalimbali jijini Mwanza asubuhi hiii wanakutana na Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka kabla ya tamasha hilo linalotarajia kufanyika Mei 4 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi hayo, Abihudi Mang’era mkutano huo utajadili mipangilio mbalimbali itakayofanikisha tamasha hilo kufanyika kwa ufanisi.

“Tumeonelea tupate mwongozo zaidi kutoka kwa Maaskofu wa Mwanza ili tufanikishe Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Mei 4 kwenye uwanja wa CCM Kirumba,” alisema Mang’era.

Mang’era alisema tamasha hilo lengo la Tamasha la Pasaka ni kusaka fedha kwa ajili ya kuwasaidia wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane sambamba na kujipanga kwa ujenzi wa kituo cha Kimataifa kitachojengwa Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete, Rafiki wa wasiojiweza.

Aidha Mang’era alitaja viingilio katika tamasha hilo jijini Mwanza ni Sh. 10,000 kwa viti maalum, viti vya kawaida Sh. 5,000 na watoto Sh. 2,000.

Kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu ni Tanzania Kwanza, Haki huinua Taifa ambayo ina lengo la kuwakumbusha wananchi kuijali na kuipenda nchi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...