Baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Shanghai nchini China wamesherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania kwa kukutana pamoja na kuzungumza mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Licha ya sherehe hizo za Miaka 50 ya Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kumaliza mwaka huu.
Baadhi ya Watanzania waishio Shanghai wakipiga picha ya pamoja katika shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanzania,yaliyofanyika jana.
Baadhi ya Watanzania wanaomaliza masomo yao mwaka huu wakipiga picha ya pamoja mbele ya keki ya Muungano.
Mmoja wa wahitimu Bi. Hellen Shayo akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Watanazania waishio Shanghai cha kuwa mwanachama hai kwa kipindi chote alichokuwa hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...