Kinana akisoma vijiji vitavyopata umeme wilayani Sikonge mwaka huu wa fedha.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia katika mkutano huo leo Mei 15, 2014, ambapo akijibu Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya Kitunda, alielezea kusikishwa kwake na kitendo cha vyama vya ushirika kudaiwa kuwadhulumu bila huruma wakulima wa tumbaku wa Kata hiyo, huku akionyesha kushangazwa kwake na hatua ya waziri mwenye dhamana na kilimo, Chakula na Ushirika kutotembelea wakulima kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Mapema baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuuliza maswali au kutoa maoni kuhusu kero walidaikuwa zaidi y asilimia 64 ya wakulima hawajapewa malipo yao ya mauzo ya tumbaku ya mwaka jana na vyama vya ushirika katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, mkoani Tabora. Pia wakulima hao walisema kuwa wanadaiwa zaidi ya sh. bilioni 112 za mauzo hewa ya pembembejeo.
Mkulima wa tumbaku katika Kata ya Kitunda, wilayani Sikonge, akielezea mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jinsi viongozi wa vyama vya ushirika walivyosaini mkataba hewa wa pembejeo zenye thamani ya s dola za kimarekani 150.
Mwakilishi wa wakulima wa tumbaku katika Chama cha Ushirika cha Tumbaku Mkoa wa Tabora ( WETCO), Lameck Mnyama, akielezea jinsi viongozi wa ushirika huo wanavyowanyonya wakulima wa zao hilo, wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kitunda uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM ambapo alidai hadi sasa wanaudai ushirika dola za kimarekani 76. Picha zaidi BOFYA HAPA
MKOA WA TABORA UMESAHAULIKA SANA SANA, UKIACHA IGUNGA NA NZEGA HAO WALIOKO HUKO NDANI KWELI HALI YA MAENDELEO SI NZURI AND NJIA MBADALA NI NYIE WATANI ZETU, MSISAHAU BARABARA!!! WAJENGE BARABARA HIYO HAIWEZEKANI MIAKA 51 YA UHURU HAMJAWAHI KUWA NA MAENDELEO. ITOKE TABORA MJINI MPAKA MPANDA WASILETE SIASA ZA MANENO MATUPU IWE KWA VITENDOOOO.....! TUMBAKU IMEANZA KULIMWA HUKO TOKA ENZI; BARABARA NI KITU MUHIMU SANA. DUH, HEBU WEWE FIKIRI TOKA PUGE KUPITIA NDALA MPAKA TABORA MJINI VUMBI.
ReplyDelete