Miss Universe Tanzania 2007 na mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata leo amejumuika na wananchi wengine mkoani Mwanza katika Ibada maalum ya kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuwaombea marehemu waliopoteza maisha yao baada ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba miaka 18 iliyopitta.
Flaviana Matata, ambaye anafanyia shughuli zake nchini Uingereza na Marekani ni mmoja wa watu waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo. Yeye alimpoteza mama yake mzazi na Kaka yake. Mbali na kusindikizwa na ndugu jamaa na marafiki pia alisindikizwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi Maajar pamoja na wasanii maarufu kadhaa akiwemo AY.
Ajali ya kuzama kwa Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamo tarehe 21/5/1996 na kupoteza maisha ya zaidi yawatu 1000.
Ukiondoa mrembo huyo Misa hiyo pia imehudhuriwa na viongozi wa dini, ndugu wa karibu wa Flaviana akiwemo baba yake Mzazi, Marafiki zake, wananchi mbalimbali na pia Viongozi wa serikali kupitia kampuni ya Marine Services Company Limited ambayo imekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.
Ibada hiyo fupi imefanyika katika makaburi ya Igoma ambapo ndipo walipozikwa na tukio hilo kama kawaida litaambatana na shughuli ya kuweka mashada ya maua na kuwasha mishumaa.
Flaviana na Balozi Mwanaidi Maajar walishiriki kuweka mashada katika mababuri
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya almaarufu kama AY alikuwepo kuungana na Flaviana Matata
Baba Mzazi wa Mwanamitindo huyo nae alikuwepo kwenye misa ya kuwaombea
Rafiki yetu mpendwa Lydia tunakukumbuka na kukuombea mapumziko mema pamoja na mwanao.
ReplyDeleteMollel
POLE FLAVIANA MATATA NAJUA MAMAKO ALIKUFA KATIKA AJARI HII MBAYA.
ReplyDeletePole sana watanzania. Lakini tuwe taari kwani hatujui siku wala saa ya kijiliwa. Tuwe taari na tujitakase na kukaa sawasawa na MUNGU aliye hai.
ReplyDelete