Napenda kukutambulisha juhudi yetu mpya inayoitwa “Najiamini Naweza” - ambayo ni matokeo ya ushirikiano kati ya Maanisha! Limited (http://www.maanisha.co.tz/) na Hivos Twaweza (http://www.twaweza.org/).
Kampeni hii imelenga kuonyesha harakati za kila siku za maisha ya Watanzania. Kampeni inahamasisha wananchi kutambua uwezo na wajibu walio nao katika kutafuta suluhu za kero/changamoto wanazokumbana nazo. Tunafahamu kwamba mabadiliko huanza na mtu mmoja na pia jinsi huyo mmoja anavyoweza kuwapa hamasa wengine waige.

Mahojiano ya “Najiamini Naweza” yalifanyika kwa kipindi cha miezi 4 - yakijumuisha wananchi wa Dar es salaam na Morogoro. Mafanikio ya kampeni hii yatatusaidia kufikia wananchi wengi na kufanya sauti zao zisikike maeneo mengine hapa Tanzania. Video zote zinapatikana katika ukurasa wetu wa Youtube: https://www.youtube.com/user/ MaanishaTV . Tanzania bora inajengwa na sisi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...