Na Teresia Mhagama
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo pamoja na
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark B. Childress wamesaini
Makubaliano ya Awali (MoU) kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Serikali ya Marekani kwa ajili ya kutekeleza mpango wa
Serikali ya Marekani wa kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme barani
Afrika, unaoitwa “Power Africa Initiative” ambao umetengewa kiasi cha
Dola za Marekani bilioni 7 na serikali ya nchi hiyo, ambapo makampuni
binafsi ya nchi hiyo yaliahidi kuwekeza Dola za Marekani bilioni 9.
Mpango huo uliozinduliwa na Rais Barack Obama wa Marekani wakati
alipotembelea Tanzania, mwezi Julai 2013, utainufaisha Tanzania pamoja
na nchi nyingine kama Ethiopia, Ghana, Nigeria, Liberia na Kenya.
Hafla ya utiaji saini makubaliano hayo ilifanyika katika Ofisi za Ubalozi
wa Tanzania Washington DC, USA mnamo tarehe 3 Agosti, 2014. Hafla
hiyo pia ilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Bi. Liberata
Mulamula.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( katikati) pamoja
na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark B. Childress (wa kwanza
kulia) wakisaini Makubaliano ya Awali kwa ajili ya kutekeleza mpango wa
Serikali ya Marekani wa kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme barani
Afrika, unaoitwa “Power Africa Initiative”. Wa kwaza kushoto ni Balozi wa
Tanzania nchini Marekani, Bi.Liberatha Mulamula.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( kushoto) pamoja na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Bw. Mark B. Childress (kulia) wakibadilishana nyaraka mara baada ya kusaini Makubaliano ya Awali kwa ajili ya kutekeleza mpango wa Serikali ya Marekani wa kusaidia maendeleo ya sekta ya umeme barani Afrika, unaoitwa “Power Africa Initiative”.
Hii ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika sekta ya nishati na kusambaza nguvu za umeme.
ReplyDelete