Mwanamuziki kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I
akizungumza na Waandishi wa Habari jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa
Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho lake la kwanza
atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini Dar katika
tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara moja,chini ya
waandaji bingwa wa burudani hapa nchini kampuni ya Prime Time Promotions
Lts sambamba na Clouds Media Group..
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Joseph Kusaga akitoa
shukurani za dhati kabisa kwa wadau mbalimbali walioshiriki kwa namna
moja ama nyingine katika kufanikisha shughuli nzima ya tamasha la
fiesta 2014, ambalo linatarajia kurindima usiku huu katika viwanja vya
leaders Club,Kinondoni jijini Dar,ambapo wasaniii mbalimbali wa ndani na
nje pia watatumbuiza jukwaani,aidha kama vile haitoshi Msanii kutoka
nchini Nigeria ajulikanae kwa jina la Davido amekiri wazi kuwa
atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha hilo,bila kikwazo chochote.
Mwanamuziki
kutoka nchini Marekani ajulikanae kwa jina la Kisanii T.I (pichani
kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) jioni ya leo
kwenye moja ya ukumbi wa Sea Cliff hotel jijini Dar kuhusiana na onesho
lake la kwanza atakalotumbuiza katika viwanja vya leaders Club,jijini
Dar katika tamasha la Fiesta 2014,ambalo hufanyika kila mwaka mara
moja,chini ya waandaji bingwa wa burudani hapa nchini,Kampuni ya Prime
Time Promotions Ltd ikishirikiana na Clouds Media Group.
Mwanamuziki
kutoka Nigeria,ajulikanae kwa jina la Davido akizungumza mbele ya
Wanahabari (hawapo pichani) kuwa atatumbuiza usiku wa leo kwenye tamasha
la Fiesta 2014 litakalofanyika usiku huu katika viwanja vya Leaders
Club Kinondoni jijini Dar.
Mdau mkubwa wa mwanamuziki T.1 kutoka Dubai ,Rasheed Sazaf a.k.a Sazaf akipeana mkono na Mwanamuziki T.I jioni ya leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...