Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akimsalimia Katibu wa CCM tawi la Kijiji cha Mkurupita, Kata ya Ndomoni, Nora Lwambano wakati alipokuwa akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa kata hiyo kwa ajili ya kuzungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo. Waziri Chikawe alitoa msaada wa madaftari na kalamu kwa ajili ya kuzisaidia shule za Msingi na Sekondari katika kata hiyo. Chikawe pia aliwaomba wajumbe hao washiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kushoto), akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Ndomoni, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo. Waziri Chikawe alitoa msaada wa madaftari na kalamu kwa ajili ya kuzisaidia shule za Msingi na Sekondari katika kata hiyo. Chikawe pia aliwaomba wajumbe hao washiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (Kulia), akimkabidhi madaftari na kalamu Diwani wa Kata ya Ndomoni, Rafael Saanane kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe yupo jimboni humo kwa ajili ya kuzungumza na kusikiliza kero za wananchi wake kupitia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM za Kata, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata za Jimbo hilo. Aidha, Chikawe aliwaomba wajumbe wa kata za jimboni kwake kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Ndomoni, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM Kata, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee katika Kata hiyo wilayani Nachingwea, Mkoa wa Lindi wakishirikiana kubeba maboksi ya madaftari na kalamu msaada uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nchingwea, Mathias Chikawe kwa ajili ya kuzisaidia Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika kata hiyo. Waziri Chikawe pia alizungumza na wajumbe hao na kuwaomba kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, akishangiliwa na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Kata ya Naipanga, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuiya zote za CCM wa Kata hiyo, Viongozi wa Dini na Wajumbe wa Baraza la Wazee wakati alipokuwa akiondoka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kata hiyo. Waziri Chikawe aliwaomba wajumbe hao kushiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na pia kuipigia kura ya ndiyo Katiba iliyopendekezwa. Picha na Felix Mwagara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. SAFI SANA MHESHIMIWA. One of the most composed Ministers...hakurupuki ila akiongea anacomand respect.

    ReplyDelete
  2. kwanini anapiga kampeni sasa hivi? Waacheni wananchi wapige kura wanavyotaka na sio kuwashawishi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...