Mtoto wa aliekuwa Waziri Mkuu wa Kenya,Raila Odinga aitwae Fidel Odinga (pichani) amekutwa akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen,jijini Nairobi mapema leo asubuhi.

Taarifa za awali zilieleza kuwa, Fidel alitoka nyumbani kwake jana usiku kwa lengo la kujumuika na marafiki zake kwa matembezi na burudani za mwisho wa wiki na alirejea nyumbani kwake alfajiri ya leo na haijulikani ni nini kilichosababisha kifo chake.

Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini Kenya,wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo hicho.

Kundi la wabunge pamoja na maseneta wa Kenya waliwasili nyumbani kwa Mh. Raila Odinga baada ya kupata habari hizo. Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa jumamosi na alikuwa na nani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. This is very sad
    Pongezi kwa familia na jamaa zake wote
    Its really sad when these people go so young so early. I remember his famous grandfather Jaramongi when he came to talk to students (Makerere) during Kenyas independence struggle. God bless him,God bless all.

    ReplyDelete
  2. Good Story na nimefurahi kwa ufuatiliaji mzuri habari hiyo imetulia. Hazina uongo kama chombeza za Wanabroger wengine.!

    ReplyDelete
  3. Wewe mtu hapo juu unatoa pongezi za kitu gani? Toa pole, huu ni msiba. Pongezi sio mahala pake hapa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...