Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiongozana na  Meneja Ufundi wa Kiwanda cha Magurudumu cha General Tyre cha jijini Arusha, Elias Pallangyo,alipofanya ziara kutembelea kiwanda hicho.
Meneja Ufundi wa Kiwanda cha Magurudumu cha General Tyre cha jijini Arusha, Elias Pallangyo,akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene , sehemu ya kiwanda hicho ambayo ipo katika ukarabati tayari kwa ajili ya uzalishaji wa Magurudumu mapema mwaka huu. Kiwanda hicho kitafufuliwa baada ya kufungwa tangu mwaka 2009.
Meneja Masoko wa Kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha, Binnesh Harrier, akimuonyesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janeth Mbene, namna fulana zinavyozalishwa kiwandani hapo juzi. Kiwanda hicho kinazalisha vyandarua, fulana zikiwemo bidhaa nyingine muhimu ambazo usafirishwa katika nchi zaidi ya 25 duniani.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha kujionea hali ya uzalishaji .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...