TIMU ya Yanga veterani imeibuka mshindi wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba veterani ulioandaliwa na PSPF, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 4-3 na kubeba kombe. Mchezo huo ulifanyika tarehe 1 Januari 2015 katika uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam.

Hadi dakika tisini zinakamilika timu hizo zilitoka sare ya bao moja kwa moja, mabao hayo yaifungwa na Omari kapilima kwa upande wa Yanga na Barnabas Sekolo kwa upande wa Simba.

Bingwa wa mchezo huo alipatikana kwa njia ya matuta, ambapo kwa upande wa Yanga walipata penalty ni Empram makoye, Ngada Shaganga, Ismail Issa na Deo Lucas. Yanga ilikuwa ikifundishwa na Peter Tino Kasongo Athumani kwa Kwa upande wa simu waliozamisha penati ni Athumani Chama, madaraka Selemani na Issa Manofu. Simba ilikuwa chini ya Kasongo Athumani.

Lengo la mchezo lilikuwa kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya ambazo Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha.
Kikosi cha Yanga.
Kikosi cha Simba.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Yanga.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu akisalimiana na wachezaji wa Simba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...