Na Veronica Simba
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Jowika Kasunga ametembelea Maonesho ya Nne ya Vito ya Arusha na kuwataka wafanyabiashara wa madini ya vito nchini kuongeza bidii na ubunifu katika kazi yao ili waweze kunufaika na biashara hiyo kwa kukuza kipato chao na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Kasunga aliyasema hayo katika siku ya kwanza ya maonesho hayo yanayofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya Mount Meru na kushirikisha wafanyabiashara wa madini ya vito wa hapa nchini na nje ya nchi.
“Kuweni wabunifu na ongezeni bidii katika kazi yenu. Msisubiri kusaidiwa na Serikali kwa kila kitu,” alisema Kasunga.
Aidha, aliwaasa kutumia fursa ya maonesho hayo kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa biashara. “Naamini maonesho haya yatawasaidia kukutana na watu mbalimbali, tumieni fursa hii vizuri.”
Maonesho hayo ya siku tatu yameanza Aprili 21, 2015 na yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, Aprili 22, 2015.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini ya Vito nchini (TAMIDA), Sammy Molel (aliyesimama), akiwaeleza Wafanyabiashara wa madini hayo utaratibu wa kushiriki katika Maonesho ya Nne ya Vito ya Arusha. Maonesho hayo yanafanyika katika Hoteli ya Mount Meru  jijini humo katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia Aprili 21 – 24, 2015.
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa madini ya vito nchini, wakimsikiliza Mwenyekiti wao, Sammy Molel (hayupo pichani) aliyekuwa akiwaeleza utaratibu wa kushiriki katika Maonesho ya Nne ya Vito ya Arusha. Maonesho hayo yanafanyika katika Hoteli ya Mount Meru
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa madini ya vito nchini, wakimsikiliza Mwenyekiti wao, Sammy Molel (hayupo pichani) aliyekuwa akiwaeleza utaratibu wa kushiriki katika Maonesho ya Nne ya Vito ya Arusha. Maonesho hayo yanafanyika katika Hoteli ya Mount Meru
 Maandalizi ya Maonesho: Sekretarieti wakiwasajili washiriki mbalimbali wa Maonesho ya Vito ya Arusha yanayofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini humo. Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi Aprili 22 na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

 Baadhi ya madini ya vito yanayouzwa na wafanyabiashara wa madini hayo katika maonesho ya vito ya Arusha, yanayofanyika jijini humo katika Hoteli ya Mount Meru kuanzia Aprili 21 – 24, 2015. Maonesho hayo yatafunguliwa rasmi Aprili 22 na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...