Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akikata utepe kuzindua safari hiyo
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akiondoa treni kwa kupunga bendera
Uongozi wa Kampuni  ya Reli Tanzania  –TRL unachukua  fursa hii kuwataarifu wateja wetu wote na Watanzania kwa ujumla na hasa ukanda  wa ziwa kuwa hatimaye ile huduma iliyokuwa ikisubiriwa leo Aprili 12 , 2015 inaelekea Mwanza ‘Rock City’ Ziwa Victoria!
Safari hii ni ya pili kwa vile ya uzinduzi iliyofanyika Aprili Mosi , 2015 ilielekea Kigoma Ziwa Tanganyika baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka. Aidhaa taarifa zinaeleza kuwa  treni hiyo ilipokelewa kwa furaha na bashasha sehemu zote ilimopita wakati wa kwenda Kigoma na kurudi Dar es Salaam.
Tayari kuna baadhi ya wakazi wa miji njiani wameutaka Uongozi wa TRL kuiruhusu treni hiyo ya Deluxe isimame katika vituo zaidi vya njiani zaidi ya vile rasmi 14 na vile vitatu vya ufundi.
Hata hivyo msharti ya uendeshaji wa huduma hii ya Deluxe unaifunga kama ilivyotolewa na Sumtra unaifunga TRL kuchukua uamuzi wa upande mmoja kwa vile uamuzi wowote hautakiwi kuathiri muda wa safari na viwango vya huduma ambazo msafiri wa Deluxe amehakikishiwa kimkataba.
Aidha safari za deluxe zitakuwa wiki mara moja siku za Jumapili itaondoka Stesheni ya Dar es Salaam saa 2 usiku ikiwa na mabehewa 15, Daraja la kawaida 10 (abiria 80 kila moja) daraja la pili la kukaa 3 (kila moja abiria 60) na daraja la pili kulala 2( kila moja watu 36). Itasimama katika vituo 17 ambavyo ni pamoja na Morogoro, Kilosa, Dodoma, Makutopora, Saranda, Manyoni, Aghondi, Itigi, Tabora, Urambo, Kaliua, Uvinza, Kigoma. Vituo vingine ni Isaka, Shinyanga, Malampaka na Mwanza. Wiki moja ikienda Kigoma wiki inayofuatia itaenda Mwanza
Kwa wasafiri wa Dodoma na Tabora hawa watatumia huo usafiri wakati wote isipokuwa wale  wanaoishia Kigoma  na Mwanza. Siku za usoni wakati mabehewa mengine ya deluxe yatapatikana safari zitakuwa kila wiki kwenda Kigoma na Mwanza.

NAULI ZA TRENI YA DELUXE  KWA MUHTASARI  KUTOKA  DAR KWENDA KIGOMA/MWANZA NIA KAMA IFUATAVYO:
Dar -Dodoma  daraja la kawaida  TZS 18,500, Daraja 2 Kukaa TZS 24, 700 Kulala: 41,200
Dar -Tabora kawaida 25,400, Daraja la 2 Kukaa 33,900 Kulala 56,500;
Dar - Kigoma kawaida 35,700, Daraja la 2 Kukaa 47,600 na Kulala 79,400 na
Dar - Mwanza ;kawaida 35,000, Daraja la 2 kukaa 46,700 na Kulala 77,800.

Aidha pia tunapenda kutoa wito wa ushirikiano wa wananchi na   wadau wote kutunza vitendea kazi na kwamba kila mmoja awe mlinzi wa mwenziwe. Tujiepushe na vitendo vya makusudi kuharibu mabehewa haya mazuri ndani na nje . Kuna msemo : KITUNZE KIDUMU’! Tukitunza vitendea kazi  vitaweza kutoa huduma kwa muda mrefu na hivyo kuongeza tija na kupunguza matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. 

Imetolewa na Afisi ya 
Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya

 Mkurugenzi Mtendaji 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunaomba na Tazara jamani, tupatieni hata ya kuishia Tunduma tu maana hilo linahitaji mkataba wa nchi mbili. Tumechoka na vifo vya mabasi tunaomba huduma za Tren ziboreshwe ili watu watumie tren badala ya mabasi yanayochinja watu kila kukicha.

    ReplyDelete
  2. TWILA KAMBANGWAApril 13, 2015

    kweli kbs tazara pia tunaomba, hata mpaka mbeya tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...