Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akikata utepe kuzindua safari hiyo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk Shaban Mwinjaka akiondoa treni kwa kupunga bendera
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unachukua fursa hii kuwataarifu wateja wetu wote na Watanzania
kwa ujumla na hasa ukanda wa ziwa kuwa
hatimaye ile huduma iliyokuwa ikisubiriwa leo Aprili 12 , 2015 inaelekea Mwanza
‘Rock City’ Ziwa Victoria!
Safari hii ni ya pili kwa
vile ya uzinduzi iliyofanyika Aprili Mosi , 2015 ilielekea Kigoma Ziwa
Tanganyika baada ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk
Shaban Mwinjaka. Aidhaa taarifa zinaeleza kuwa treni hiyo ilipokelewa kwa furaha na bashasha sehemu
zote ilimopita wakati wa kwenda Kigoma na kurudi Dar es Salaam.
Tayari kuna baadhi ya wakazi
wa miji njiani wameutaka Uongozi wa TRL kuiruhusu treni hiyo ya Deluxe isimame
katika vituo zaidi vya njiani zaidi ya vile rasmi 14 na vile vitatu vya ufundi.
Hata hivyo msharti ya
uendeshaji wa huduma hii ya Deluxe unaifunga kama ilivyotolewa na Sumtra unaifunga
TRL kuchukua uamuzi wa upande mmoja kwa vile uamuzi wowote hautakiwi kuathiri
muda wa safari na viwango vya huduma ambazo msafiri wa Deluxe amehakikishiwa
kimkataba.
Aidha safari za deluxe
zitakuwa wiki mara moja siku za Jumapili itaondoka Stesheni ya Dar es Salaam
saa 2 usiku ikiwa na mabehewa 15, Daraja la kawaida 10 (abiria 80 kila moja)
daraja la pili la kukaa 3 (kila moja abiria 60) na daraja la pili kulala 2(
kila moja watu 36). Itasimama katika vituo 17 ambavyo ni pamoja na Morogoro,
Kilosa, Dodoma, Makutopora, Saranda, Manyoni, Aghondi, Itigi, Tabora, Urambo,
Kaliua, Uvinza, Kigoma. Vituo vingine ni Isaka, Shinyanga, Malampaka na Mwanza.
Wiki moja ikienda Kigoma wiki inayofuatia itaenda Mwanza
Kwa wasafiri wa Dodoma na
Tabora hawa watatumia huo usafiri wakati wote isipokuwa wale wanaoishia Kigoma na Mwanza. Siku za usoni wakati mabehewa
mengine ya deluxe yatapatikana safari zitakuwa kila wiki kwenda Kigoma na
Mwanza.
NAULI ZA TRENI YA DELUXE
KWA MUHTASARI KUTOKA DAR KWENDA KIGOMA/MWANZA NIA KAMA IFUATAVYO:
Dar -Dodoma daraja la kawaida TZS 18,500, Daraja 2 Kukaa TZS 24, 700
Kulala: 41,200
Dar -Tabora kawaida
25,400, Daraja la 2 Kukaa 33,900 Kulala 56,500;
Dar - Kigoma kawaida
35,700, Daraja la 2 Kukaa 47,600 na Kulala 79,400 na
Dar - Mwanza ;kawaida
35,000, Daraja la 2 kukaa 46,700 na Kulala 77,800.
Aidha pia tunapenda kutoa
wito wa ushirikiano wa wananchi na
wadau wote kutunza vitendea kazi na kwamba kila mmoja awe mlinzi wa
mwenziwe. Tujiepushe na vitendo vya makusudi kuharibu mabehewa haya mazuri
ndani na nje . Kuna msemo : KITUNZE KIDUMU’! Tukitunza vitendea kazi vitaweza kutoa huduma kwa muda mrefu na hivyo
kuongeza tija na kupunguza matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.
Imetolewa na Afisi ya
Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Mkurugenzi
Mtendaji
Tunaomba na Tazara jamani, tupatieni hata ya kuishia Tunduma tu maana hilo linahitaji mkataba wa nchi mbili. Tumechoka na vifo vya mabasi tunaomba huduma za Tren ziboreshwe ili watu watumie tren badala ya mabasi yanayochinja watu kila kukicha.
ReplyDeletekweli kbs tazara pia tunaomba, hata mpaka mbeya tu
ReplyDelete