Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana
Kissiok Ole Mbille Lukumay kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za
Zabuni za Umma.
Aidha,
Rais Kikwete amemteua Bwana Onesmo Hamis Makombe kuwa
Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.
Taarifa
iliyotolewa Alhamisi, mjini Dar es Salaan na Ofisi ya Katibu
Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa maofisa hao
wawili ulianza Ijumaa ya Machi 27, 2015.
Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Lukumay ambaye ana diploma in Materials Management na ni
Certified Supplies Professional na pia ana MBA (Procurement and Logistics) alikuwa
Ofisa Ugavi Mkuu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za
Umma.
Naye
Bwana Makombe kabla ya uteuzi wake alikuwa Kaimu Kamishna, Kitengo cha Kudhibiti
Biashara ya Fedha Haramu. Kielimu, Bwana Makombe ana shahada za B.Com, CPA na
MBA (Finance
and Human Resources Management).
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
10
Aprili,2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...