Pichani ni uwanja wa Mwembe Yanga Temeke wakati wa Shindano la Shika ndinga ya 93.7 EFM kwa wilaya hiyo lililofanyika Jumamosi tarehe 18 mwezi wa nne mwaka 2015 ambapo washiriki kumi
kutoka wilaya hiyo wamefuzu kuingia fainali ya shika ndinga kwa mkoa wa Dar-es-salaam
kati yao watano wakiwa wanawake na wengine watano ni wanaume.Shindano hili kwa
wilaya hii lilikuwa la aina yake ukilinganisha na wilaya zingine kwa maaana washiriki
walishika ndinga huku mvua kubwa ikinyesha jambo ambalo liliongeza ushindani
baina yao.
Shika ndinga ni shindano la aina yake linaloandaliwa
na redio ya 93.7 EFM kama namna ya kutoa
shukurani kwa wasikilizaji kwa ushirikiano wao ndani ya mwaka mmoja tangu
kuanzishwa kwa redio hiyo ,ambapo washiriki wanatakiwakusikiliza redio ya EFM
na kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na redio hiyo ili kupata nafasi ya
kushika ndinga ya gari ya biashara inayojulikana kama kirikuu kwa muda
uliopangwa bila kutikisika, kuyumba ama kutetemeka na mshindi kujishindia gari
hiyo ya biashara.
Mchakato wa shindano nzima ulikuwa hivi, wanaume
walishika ndinga moja na wanawake pia walishika ndinga moja
wakiwa wamesimama kwa miguu miwili kwa masaa kadhaa na badae walishika ndinga
wakiwa wamesimama na mguu mmoja na hatimaye watano katika kila kundi
walifanikiwa kuingia kwenye fainali ambayo itawahusisha washindi wa shika
ndinga wa wilaya zote tatu yani ilala , kinondoni na temeke ambao kwa pamoja
watashindana kujishindia ndinga ya biashara .fainali ya shika ndinga itafanyika
jumapili ya tarehe 26 mwezi huu wa nne hivo watu wengi wajitokeze ili
kushuhudia shindano hili la aina yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...