MKAZI wa Heka wilayani Manyoni Mkoani Singida Joha Athumani(pichani), anaomba wasamaria wema kumsaidia msaada wa matibabu kwaajili ya mtoto wake Halima Mohamed mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anayesumbuliwa na tatizo la kutoona.
Akizungumza na ripota wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati, Joha alisema kutokana na uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni zinahitajika fedha zaidi ya shilingi laki tano (500,000/=) kwaajili kufanyiwa upasuaji mtoto huyo.
Alisema kwasasa hana uwezo wa kumtibia mtoto huyo kutokana kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili mtoto huyo aweze kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo alisema kwa sasa hana msaada wowote kutokana na mumewe kumkimbia baada ya kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo.
Mkazi huyo wa Heka alisema mwanaye alianza kusumbuliwa na tatizo la kutoona akiwa na umri wa miezi mitatu mpaka sasa, ambapo amezunguka huku na huku lakini hajafanikiwa kupata matibabu ya mtoto wake.
Ameomba wasamaria wema watakaoguswa kumsaidia, wawasiliane na mwandishi wa gazeti hili kupitia namba 0712 561279.
Barua ya rufaa aliyoandikiwa Joha Athumani ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu ya mwanaye Halima Mohamed.
Pole sana dada,
ReplyDeleteLabda ningeweza kusaidia na kiasi kidogo lakini laki tano sina mwenyewe. Je, bado unahitaji kiasi gani? Kwa mawasiliano zaidi nitumie tu e-mail: gromobir [AT] arcor [Dot] de
Msaada wa mawazo, ccrbt wamejikita kwenye mambo ya macho na watoto wadogo kama wake wanapata huduma bure. Angeshauriwa kuomba muhimbili wampeleke ccbrt
ReplyDelete