Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akifungua pazia kama ishara ya kuifungua Barabara ya Wete- Gando na Wete-Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba akiwa katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo,(kushoto) Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Issa Haji Ussi (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Juma Malik Akili (wa pili kushoto) na Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban wakitembea katika Barabara ya Wete-Gando baada ya kuizinduliwa rasmi juzi,katika katika ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo Mkoa wa Kaskazini Pemba.
[Picha na Ikulu.]
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...