Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka atapanda ulingoni mjini Manchester Uingereza Novemba 7 kupambana katika pambano lisilokuwa la ubingwa.

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Advance Security Limited, Juma Ndambile amesema kuwa Cheka anatarajia kuondoka wiki ijayo kwa ajili ya pambano hilo.

Ndambile ambaye ni meneja wa Cheka, alisema kuwa tayari msaidizi wake, Rashid Nassoro yupo nchini Uingereza akiwa na mabondia wengine wawili huku akikamilisha maandalizi ya mwisho ya pambano hilo.

Kwa mujibu wa Ndambile, Cheka anaweza kupambana na mpinzani wake wa awali, Martin Murray au bondia mwingine kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi.

 “Maandalizi yanaendelea vizuri na msaidizi wangu, Rashid Nassoro, kwa sasa yupo Uingereza akikamilisha masuala ya pambano hilo, kuna vitu fulani fulani vilikuwa havijakamilika, ila pambano ni Novemba 7 na leo jioni nitajua lini tutaondoka Tanzania,” alisema Ndambile ambaye kwa sasa yupo Kenya kikazi.

Alisema kuwa Cheka kwa sasa yupo mkoani Morogoro akiendelea kujiandaa na pambano hilo na kama unavyojua, akishinda, atapata ofa kubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa.

Alisema kuwa Cheka anatakiwa kushinda pambano hilo ili kusaini mkataba mnono wa zaidi ya dola za Kimarekani 25,000 (Sh milioni 50) ili kupigana katika pambano linalofuata la ubingwa “Lengo ni kumfanya bondia bora ili hata akiachana na masumbwi ya kulipwa, awe na maisha mazuri, chini yangu pia nitamfundisha jinsi ya kuwekeza katika biashara na kujipatia kipato, nilisikitishwa sana matatizo aliyopata,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa Cheka amekuwa na heshima kubwa hapa nchini na ghafla heshima hiyo kupotea kutokana na mambo ya ‘kidunia’ na yeye ameakua kumkwamua kabisa.

Wakati huo huo; Bondia Benki Mwakalebela ambaye alitakiwa kupanda jukwaani jana usiku, hakuweza kufanya hivyo baada ya pambano lake kuhairishwa dakika za mwisho.

Ndambile alisema kuwa Mwakalebela alitakiwa kupambana na bondia Craig Kennedy na pambano hilo limefutwa kutokana na sababu za kiufundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. michuzi blog HEBU TUSAIDIENI. HII NI SCHEDULE BBA ITAKAYOFANYIKA NOV 7, ECHO ARENA MJINI LIVERPOOL NA ITAONYESHWA LIVE ON SKY SPORTS. NIMEANGALIA HAKUNA JINA LA CHEKA NA WALA HAKUNA BOXING EVENT IN MANCHESTER. HII NI KW SABABU ALL BOXING OFFICIALS WATAKUWA LIVERPOOL. NIMEAMBATANISHA NA KIELELEZO CHA RATIBA YA TAREHE 7 HUKO LIVERPOOL. MSAADA TUTANI TUNATAKA TUKAMUONE MBONGO AKIMTOA MZUNGU MANUNDU....

    07/11/2015
    ECHO ARENA, LIVERPOOL
    Callum Smith and Rocky Fielding will clash for the vacant British Super Middleweight title in an all-Liverpool blockbuster at the Echo Arena on November 7, live on Sky Sports.

    The unbeaten Liverpool stars have been on a collision course following their impressive wins in June, with Fielding blasting away World rated Texan Brian Vera inside two rounds and Smith outpointing former European champion Christopher Rebrasse

    SCHEDULE
    CALLUM SMITH VS ROCKY FIELDING
    12 x 3 mins British & WBC Silver Super Middleweight Titles

    SCOTT CARDLE VS SEAN DODD
    12 x 3 mins British Lightweight Championship

    RICKY BURNS VS JOSH KING
    12 x 3 mins WBO Inter-Continental Lightweight title

    TOM DORAN VS ROD SMITH
    10 x 3 mins Eliminator for British Middleweight title

    O'HARA DAVIES VS CHRIS TRUMAN
    8 x 3 mins Lightweight contest

    JAKE BALL VS TBA
    6 x 3 mins Light-Heavyweight contest

    RYAN MULCAHY VS TBA
    4 x 3 mins Flyweight contest

    MARC LEACH VS IAN HALSALL
    4 x 3 mins Bantamweight contest

    NO MURRA NO NOTHING.....

    ReplyDelete
  2. "NO MURRA NO NOTHING....." but there is TBA which means to be announced.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...