Mbunge Mteule wa jimbo la Mafinga Mjini Ndugu Cosato Chumi akiwa amebebwa na wananchi wa Kijiji cha Isalavanu wakati wa ziara yake ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa kura za wingi.
Ndugu Chumi ametembelea jumla ya Vijiji 15 kwa muda wa siku mbili katika kata za Bumilayinga, Sao Hill, Isalavanu na Rungemba. Baada ya kuapishwa ataendelea katika kata zilizosalia ambazo ziko katikati ya Mji wa Mafinga. Mhe. Chumi amesema yeye sasa ni mbunge wa wote waliompa kura na hata ambao hawakumpa kura, wana CCM na hata wasio wana CCM, wenye vyama na hata wasiokuwa na vyama. Na kwamba Hapa Kazi Tu!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...