Bwana Harusi Said akimnywesha Shampein mkewe Salma wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika kwenye Uukumbi wa Best Choice uliopo Tabata jijini Dar es Salaam, jana usiku ambapo wanandoa hao walijiwekea historia ya ndoa yao kwa kusherehekea siku maalum ya utambulisho wa Rais mpya wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli aliyekabidhiwa hati ya utambulisho wa ama cheti cha ushindi kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliomalizika wiki iliyopita.
Aidha wanandoa hao walifunga Ndoa Okt 27 huko Karatu mkoani Arusha.
Bi Harusi Salma akimlisha Keki mumewe Said ikiwa ni ishara ya upendo.
Bwana harusi na Bi Harusi,wakimkabidhi keki Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe yao, George John, ikiwa ni sehemu ya kumshukuru kwa kusheresha na kufanikisha sherehe hiyo.
Mdogo wa Bi harusi akifanya yake ukumbini hapo...
Bw na Bi Harusi wakiwa katika pozi....
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...