Balozi wa maziwa makuu nchini Kenya katika
wizara ya mambo ya nje, Mhe. Muburi Muita(aliyenyoosha mikono) akiongea na Katibu
mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel
wakati alipomtembelea ofisini kwake na ujumbe wa kutoka eneo la maziwa
makuu(ICGLR) waliokuja kuangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa
Tanzania na kuelezea kufurahishwa na ushiriki wa vijana wengi katika uchaguzi
huu na kwamba uchaguzi ulikuwa wa Amani na mafanikio makubwa.Ujumbe huo
unajumuisha nchi za Zambia,Burundi,Kenya,Congo,Uganda na Sudan.
Katibu
mkuu wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel(wa
pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maziwa makuu ambao upo
nchini ukiangalia ushiriki wa vijana katika uchaguzi mkuu wa Tanzania.Wengine
kwenye picha ni Balozi wa maziwa makuu
nchini Kenya katika wizara ya mambo ya nje, Mhe. Muburi Muita(wa kwanza Kushoto
waliokaa) na Nancy Kaizilege wa Umoja wa mataifa Tanzania.(wa kwanza kulia
waliokaa).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...