Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya Mkurungenzi wa manispaa ya Iringa  pamoja na mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji  Peter Msigwa.

Katibu wa CCM  wilaya ya Iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema kuwa taarifa zilizosambaa sehemu mbalimbali sio za kweli.
“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya 2015 haijafutwa”alisema Mwampashe.
Ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuiendesha hivyo anashangaa kuaona taarifa zinazendelea kuena mitaani.
“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la msingi  ambalo lilikuwa na kupinga matokeo na kuna  shauri dogo  namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria kuruhusu kufanya hivyo” alisema Mwampashe.
Amewataka wananchi  na wanachama wa CCM kuendelea kuwa na subira kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani, na amewasihi wananchi wanaopotosha taarifa hizi waache mara moja. 
Kwa upande wake Fredrick Mwakalebela, aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.
“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na Mkurugezi wa manispaa ya Iringa pamoja na mchungaji Peter msingwa” alisema mwakalebela, na kuongezea 
kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye pamoja na  CCM  kwa kuwa ndio kilichompa nafasi ya kugombea ndio maana kila kitu anachokifanya chama lazima kijue, hususan mwenendo wa kesi hivyo. 

Hii inafuatia kutolewa taarifa kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa mjini.
Msajili wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema mgombea ubunge jimbo La Iringa mjini Fredrick Mwakalebela aliomba kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo, kwa mujibu wa  vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo.

 Hata hivyo mahakama ilikataa na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake kwa gharama hiyohiyo.

Hivyo uvumi uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado haijapangwa wala kuanza kusikilizwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...