Michuano ya Kombe la Shirikisho ya (Azam Sports Federation Cup) itafunguliwa rasmi kesho Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti, ambao jumla ya timu 64 zitashirki kuwania nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
 Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.


SDL KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 15
Ligi Daraja la Pili nchini (SDL) inatarajiwa kuanza kutimua vumbi wikiendi ijayo Novemba 15 katika viwanja mbalimbali nchini, huku timu 24 zinazoshiriki ligi hiyo zikisaka nafasi nne za kupanda ligi Daraja la Kwanza (FDL) msim ujao.  Fuata link chini kwa taarifa zaidi

STARS KUJIPIMA NA U23 YA AFRIKA KUSINI
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya vijana wenye umri chini ya miaka 23 (Amaglug-glug) Jumanne jioni kwenye dimba la Eldorado jijini Johannesburg. Fuata link chini kwa taarifa zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...