Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga akitoa maelezo jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi zake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (kulia) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. (Picha na Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
Kutoratibiwa kwa mbegu za alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika kuendesha viwanda vyao kwa gharama nafuu.
Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez.
Mratibu huyo alikuwa Dodoma kwa shughuli mbalimbali za ukaguzi wa miradi pamoja na kuhudhuria shughuli za bunge la Tanzania lililomalizika jana.
Timothy alisema kwamba pamoja kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa mbegu za kutosha nchini Tanzania,hali halisi inayoelezwa na wasindikaji inaashiria kwamba sekta hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila kuwa na mbegu za kusindika.
Aidha alisema kwamba mbegu za alizeti zinazovunwa kuanzia Aprili hadi Julai na huwa na bei nafuu kipindi hicho lakini kama wasindikaji wakikosa mitaji na kununua mbegu chache, msimu unapoisha hawawezi tena kuendelea kufungua viwanda vyao.
Alisema kwamba wasindikaji hao wanakumbana na kiwango kikubwa cha riba kuanzia asilimia 20 kwenda juu , riba ambayo inakwamisha maendeleo ya viwanda hivyo.
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa pili kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (wa pili kulia) wakipata picha ya ukumbusho katika matanki ya kuhifadhia mafuta ya alizeti kiwandani hapo.
Hizi ndio kazi Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linapaswa kufanya. Maendeleo yanayoonekana sio semina na workshops tu. Hapa kazi tu.
ReplyDelete