
KIKUNDI cha wakinamama kijulikanacho kwa jina la Victory Women Group (VWG) chenye makao yake makuu jijini Dar es salaam, mwisho mwa wiki, kilijumuika pamoja na kuwapatia msaada wa mahitaji mbali mbali watoto Yatima wanaolelewa kwenye Kituo cha CHAKUWAMA, kilichopo Sinza Mori jijini Dar es salaam.
VWG iliamua kutembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yake ya kutimiza mwaka mmoja toka kuanzishwa kwake.
Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo, Mwenyekiti wa VWG, Bi. Consolata Maimu, alisema kuwa waliamua kufanya hivyo kwa kuwa wao ni kina mama na wanahofu ya Mungu hivyo wakaona ni vyema kujumuika na watoto hao kuliko kwenye kusherehekea wenyewe.
VWG ni kikundi cha wanawake kilichoanzishwa mwezi mei 2014, kikiwa na lengo la kusaidiana wao wenyeke katika kujikwamua na umaskini na pia kusaidia jamii inayowazunguka, huku lengo lingine likiwa ni kuwasomesha watoto wanaolelewa kwenye vituo mbali mbali kwa kuanzaia elimu ya Sekondari mpaka Chuo kikuu.
Mwenyekiti wa Kikundi cha wakinamama kijulikanacho kwa jina la Victory Women Group (VWG), Bi. Consolata Maimu (katikati), akikabidhi kwa Mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hassan Hamis, sehemu ya sare za shule kwa ajili ya watoto wanaolelewe kwenye kituo hicho, ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na kikundi hicho. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha VWG, Bi. Sauda Sinare.
Mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hassan Hamis, akizungumza machache mbele ya wageni wake, juu ya hali ya kituo hicho.
Mwenyekiti wa Kikundi cha wakinamama kijulikanacho kwa jina la Victory Women Group (VWG), Bi. Consolata Maimu akizungumza katika hafla hiyo.
Sehemu wa wanachama wa Kikundi cha wakinamama kijulikanacho kwa jina la Victory Women Group (VWG), wakijumuika pamoja na watoto Yatima wa kituo cha CHAKUWAMA kukata keki na kufungua shampein.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...