
Matamasha
hayo ambayo yatafanyika wilaya za Tukuyu, Ruangwa, Moshi Vijijini, Chato pamoja
na Mpwapwa, yatajumuisha wasanii wa bongo fleva pamoja na burudani nyingine
kutoka kwa wasanii wa maeneo hayo.
Tamasha
la Halo Christmass wilayani Tukuyu litafanyika katika uwanja wa Tandale na
burudani itatolewa na wasanii Tundaman na Makomando.
Kwa
upande wa Ruangwa, tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Likangala, na kutumbuizwa na wasanii Amini pamoja na Matonya, wakati Mpwapwa tamasha
litafanyika katika viwanja vya Mgambo likitumbuizwa na wasanii Madee na
Malaika.

Wakazi
wa Moshi vijijini pia watafurahia tamasha la Christmass kwa burudani Shilole na
Msami zitakazofanyika katika viwanja vya Kae.
Akizungumzia
matamasha hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Halotel bwana Nguyen Thanh
Quang, amesema matamasha hayo ya
Halotel yanalenga kuwaleta watumiaji wa Halotel pamoja na kuwapa burudani ya
kufunga mwaka.
‘Hii ni zawadi kwa watumiaji wa mtandao wetu na
wateja wapya wanaotaka kujiunga na familia yetu ya Halotel, na ndio maana
tunawafata katika maeneo yao yalipo’ alisema Quang.

Quang pia amewaahidi wateja wa Halotel kuwa mtandao
wake unatarajia kuleta mabadiliko katika sekta ya mawasiliano nchini kwa kuwapa
wateja wake zaidi ya huduma za simu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...