Sehemu ya kwanza: Utangulizi na Chimbuko la Makala

Miezi kadhaa iliyopita, niliamka asubuhi na mapema kuwahi mkutano ambao nilikwenda  kuhudhuria katika jiji la London, Uingereza. Kwa kuwa nililala nje kidogo ya jiji hili lenye watu kadiri ya milioni kumi, na kwa kua ni mbali kidogo kutoka nilipokua nahudhuria mkutano, nililazimika kupanda treni kwa muda usiopungua kama dakika arobaini hadi nifike kituo cha Euston kilicho chini ya ardhi (underground) na ambapo sio mbali sana na nilipokua naelekea. 

Kama kawaida ya London wakati wa asubuhi, treni hujaa sana watu wakielekea makazini, kwenye utalii, na shughuli zingine. Nililazimika kusimama kwa kuwa hapakua na pa kuketi na abiria wengine wengi tu walisimama. Nilirusha macho mbele na nyuma, kushoto na kulia: na nilichokiona ni wingi wa watu waliofunikwa na ukimya wa ajabu. Sikuona mtu akiongea na mwingine wala wanaoingia wakisalimiana na wanaowakuta ndani, kitu ambacho ni tofauti sana na nilivyozoea kule kwetu uswahilini. 

Nakumbuka miaka sio mingi, kwetu uswahilini ilikua kawaida kusalimiana na kila mtu hata kama hamujuani na kama ni kwenye chombo cha usafiri munaweza kupiga stori au kujadili matukio yaliyokamata vichwa vya habari kwa uhuru na kujiachia kama vile mumelala nyumba moja au mumefahamiana kwa miaka miwili iliyopita. 

Kumbe, ndio kwanza munaonana kwa mara ya kwanza na hamujuani hata majina; na hadi mutakapoachana huenda hakuna atakayemuuliza mwenzake anaitwa nani au yeye ni nani au anafanya nini. Mara chache ungeweza kua na bahati ukute unayeongea naye katoka ng’ambo ya Ziwa Victoria kwani ndani ya dakika chache utajua anaitwa nani, ana shahada ngapi na za nini, na iwapo pasipoti yake imejaa au la kutokana na wingi wa safari za Ulaya na Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...