MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.

Mwaitege alisema Tamasha la Pasaka lina ujumbe wa Mungu hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi na kumkimbilia M
ungu katika tamasha hilo.

“Watanzania tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kwa sababu Yesu alikufa na kufufuka, hivyo kuna kuna ujumbe mkubwa kutoka kwa Mungu ambao utawaokoa Watanzania wote,” alisema Mwaitege. 

Mwaitege alisema kupitia tamasha hilo jamii inaondokana na machafu ambayo yanamchukiza Mungu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha la mwaka huu wamejipanga vilivyo kufanikisha matakwa ya jamii kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili na viongozi wa dini watakaohudhuria tamasha hilo.

Msama alisema tamasha la mwaka huu wamepanga litaanza Machi 26 hadi 28 hapa nchini, hivyo Watanzania wajiandae na tamasha hilo.

“Watanzania watarajie tamasha bora ambalo litafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii, hivyo wajiandae,” alisema Msama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...