Na Skolastika Tweneshe-Maelezo
Jiji la Dar es salaam limeripotiwa kutokuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu kuanzia Desemba mwaka jana.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mh. Dkt Hamisi Kigwangalla amesema kuwa licha ya ugonjwa wa kipindupindu kuanzia jijini Dar es salaam na kudumu kwa miezi mine lakini kuanzia kwa sasa hajaripotiwa mgonjwa wa kipindupindu.
“Mkoa wa Dar es salaam ambako ndipo ugonjwa ulipoanzia na kudumu kwa miezi minne haujaripotiwa kuwa mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015,” alisema Kigwangalla.
Waziri aliongeza Kigwangalla aliongeza kuwa mikoa mingine ambayo haijaripotiwa kuwa na maambukizi kwa muda wa wiki moja ni pamoja na Mbeya,Rukwa,Katavi,Kigoma,Kagera na Lindi.
Aidha alisema kuwa mikoa ambayo haijarioptiwa ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa pia amesema kuwa kuna mikoa ambayo haijawahi kuripoti ugonjwa wa kipindupindu uanze nayo ni mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara.
Dkt. Kigwangalla alisema mikoa iliyotoa idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu ambayo ni Halmashauri ya Morogoro(66), Arusha (50), Singida(40), na manispaa ya Dodoma (33).
Pia amewaasa wananchi kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama pamoja na kunawa mikono na maji safi na sabuni kwa maji safi yanayotiririka pamoja na kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji ,maziwa na mabwawa.
Kwa mujibu wa wizara ya afya tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua kipindupindu, na kati yao watu 205 wameshafariki kutokana na ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala (kushoto) akitoa taarifa ya hali ya ugonjwa wa kipindupindu nchini katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo jijini Dares Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya la Dunia(WHO), Dkt .Rufaro Chotaro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya(kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa huo.Kulia ni Waziri wa wizara hiyo Dkt. Hamis Kigwangala.
(Picha kwa hisani ya Wizara ya Afya)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...