Waziri mkuu wa zamani na aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA na kuungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa amempongeza mwanasoka wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kwa kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Samatta alichaguliwa jana usiku huko Nigeria kuwa mwanasoka bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza soka barani humu.

Katika pongezi zake, Lowassa ambaye ni mshabiki wa soka asiyependa kuweka wazi anapenda Simba au Yanga, amesema ushindi wa Samatta ni changamoto kubwa kwa wana soka wa tanzania lakini zaidi kwa Serikali kuwekeza kwenye eneo hilo.

"Huyu kijana kufikia hapo ni kujituma kwake, lakini zaidi ni malezi aliyoyapata katika timu yake ya TP Mazembe...ni lazima tuwe na utaratibu wa kujenga shule za kukuza vipaji vya soka (academy), tutawapata kina Samatta wengi" alisema Lowassa.

Ameongeza kuwa serikali isione shida kuchukua ilani ya CHADEMA iliyoridhiwa na UKAWA ambayo inataka kufutwa kodi kwa vifaa vyote vya michezo.

"Wasione haya kuchukua ilani yetu. sisi tulitangaza kuwa tutafuta ushuru kwa vifaa vyote vya michezo pamoja na kuanzisha Academy ilikuinua vipaji, tunaamini kwa kufanya hivyo watapatikana kina Samatta wengi tu na si katika soka, bali hata michezo mingine kama riadha na ngumi" alisisitiza na kuongeza.

"Kumpongeza tu pekee yake hakutasaidia hawa wengine, ni lazima kuwe na mikakati ya kuwaendeleza vijana wetu hawa. Huwa sipendi kuona wachezaji kutoka nje ndiyo wanaotamba katika timu zetu kubwa, wakati kuna vipaji vingi sana...Kama tukiviendeleza itakuwa kama Brazil au Nigeria..wa nje ndiyo waje kuchukua wachezaji hapa" ameshauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...