Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza amewataka wanawake wa Wilaya ya Mbozi na mkoa kwa ujumla kumtumia ipasavyo kuwasilisha kero zao ili akawapiganie bungeni kwani ndio kazi alioomba.

Shonza alitoa rai hiyo jana wakati akitoa shukrani zake kwa wajumbe wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Mbozi, mkoani hapa kumuamini na kumpatia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana kupitia chama hicho.

Alisema kama walivyomuamini kwa kumpatia kura nyingi zilizomuwezesha kupata ubunge, ndivyo wanavyotakiwa kumtumia katika kipindi chote cha uongozi wake huku akiomba ushirikiano wa dhati kutoka kwao (wananchi) kwenye utekelezaji wa majukumu ya kijamii ikiwamo miradi mbalimbali anayotarajia kuifanya.

Shonza alisema anafahamu changamoto zinazowakabili wananchi wa Mbozi,ikiwamo umeme hususani vijijini, pembejeo za kilimo, maji na mawasiliano hivyo wampe ushirikiano na anakwenda bungeni kupigania mambo hao muhimu kwani mawaziri wengi ‘anawamudu’.

Aliwataka wananchi hao kujiunga kwenye vikundi iwe rahisi kusaidiwa kwa kupatiwa mikopo na misaada mingine ambayo itawasidia kukuza vipato vyao, kwani huu ni muda wa kuwezeshana hususani wanawake ambao ndio nguvu kuu ya familia.

Alisema ‘Hivi sasa huwezi kupata mkopo mtu binafsi ni lazima ujiunge kwenye kikundi, hivyo basi leo kwa kuanzia natoa Sh600,000 kwa ajili ya kusajili vikundi vyenu, kwa vile ambavyo vipo tayari lakini hamjavisajili. Ila huu ni mwanzo tutafanya mambo mengi na mazuri zaidi’.

Mwenyekiti wa UWT, Wilaya ya Mbozi, Issabela Mbaya alisema umoja huo utamtumia Shonza kuleta umoja na maendeleo kwa wanawake wa wilaya hiyo.
Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza, akizungumza na Wajumbe wa Jumuiya ya wanawake wa CCM, (UWT) wilaya ya Mbozi, jana mchana mjini Vwawa, wilayani Mbozi, Shonza alikutana na wajumbe hao kwa lengo la kutoa shukrani zake kumuamini na kumpatia ubunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.
Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Songwe, Juliana Shonza,(mwenye nguo nyekundu) akicheza na Wajumbe wa Jumuiya ya wanawake wa CCM, (UWT) wilaya ya Mbozi, jana mchana mjini Vwawa, wilayani Mbozi, Shonza alikutana na wajumbe hao kwa lengo la kutoa shukrani zake kumuamini na kumpatia ubunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nawaona wakina mama waki ji mwaya mwaya, wanawake wamepewa fursa kubwa sana kisiasa bongoland, actually kuna nchi huku ulaya ambazo hawana wanawake wengi serikalini na bungeni kama ilivyo Tanzania, well done and keep it up!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...