Usiku wa kuamkia leo, staa wa muziki wa Bongo Fleva, Pamela Daffa 'Pam D' kwa kushirikiana na mtayarishaji na mwanamuziki hatari Bongo, Mesen Selekta walikinukisha vya kutosha ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama jijini Dar.

Usiku huo uliotawaliwa na redcarpet ya hatari ambapo mashabiki kibao walipata nafasi ya kupiga picha na Pam sambamba na kuzungumza naye mawili-matatu, ulianza kwa kwa Mesen kupanda na kundi zima la Team Selekta ambapo alipopanda Mesen aliwapagawisha vilivyo na ngoma zake zote kali kama vile Kanyaboya, Sweetlove, Team Selekta pamoja na wimbo wake mpya wa Love Me.

Shangwe zilizidi pale walipopanda madensa wa PAm D kwa sarakasi kibao na madoido ambapo Pam alitokelezea na kuanza kuvurumusha nyimbo zake zote kali kuanzia Nimempata kisha akamalizia na Popo Lipopo ambapo mashabiki walipata fursa ya kuuona kwa mara nyingine live ukumbini hapo.
PAM D (70) Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa akiwaburudisha mashabiki waliojitokeza kwenye uzinduzi wa video yake ya Popo Lipopo ndani ya Maisha Basement usiku wa kuamkia leo.
PAM D (75)Pam D (mwenye kipaza sauti) akichana freestyle mbele ya mashabiki wake.
PAM D (64)Madensa wa Pam D wakiendelea kufanya yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...