![]() |
Mbwana Ally Samatta akiwa amejipumzisha akiwa kajifunika bendera ya Taifa baada ya kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora kwa wanasoka wanaochezea Barani Afrika |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI.
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salam za pongezi Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Nnauye kufuatia mchezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) Mbwana Ally Samatta kutwaa tuzo ya Mchezaji
Bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika; iliyotolewa katika mji
wa Abuja nchini Nigeria jana usiku.
Mhe. Rais Magufuli
amemtaka Waziri Nape Nnauye amfikishie salam zake za pongezi kwa mchezaji huyo
ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo DRC) .
Amesema tuzo hiyo
imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa
nchini na Tanzania kwa ujumla katika medani ya Soka Kimataifa.
Aidha, Rais Magufuli
amewasihi wachezaji wa soka wote na wadau wa mchezo huo kuongeza juhudi za
kuundeleza mchezo huo ili upige hatua zaidi za kimaendeleo.
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es Salaam
08 Januari,
2016.
Hongera sana kaka Mbwana kwa kuipeperusha bendera ya taifa letu vyema.
ReplyDeleteMungu akubariki na akuongezee afya na ujuzi zaidi.