Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Bw. Raphael Hokororo, wakionesha kwa waandishi wa Habari picha rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt John Pombe Joseph Magufuli leo Ijumaa January 8, 2016. Picha hiyo inauzwa kwa sh. 15,000/- tu.
Na Zainabu Hamis, Globu ya Jamii.
PICHA Rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuri imetoka leo Januari 8, 2015 katika Ofisi ya Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo Bi. Zamaradi Kawawa, amesema kuwa Picha hiyo ya Rais Magufuri kwa kila moja itauzwa kwa sh15000/- ya Kitanzania bila ya kuwekwa frem, huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa kwa sh 5000/-.
Aidha Bi. Kawawa amesema kuwa nakala za picha hizo zinapatikana Idara ya Habari Maelezo na Ofisi za Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA).
Amesema picha hiyo ya Rais pamoja na ya Baba wa Taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali,Taasisi za Umma, Mashirika na Ofisi Binafsi.
Aidha Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Maelezo Raphael Hokororo amesema picha ya Rais Magufuri imewahi kutoka mapema sana kuliko picha za Waheshimiwa waliopita na kusema kuwa hairuhusiwi kukopi wala kunakili picha hiyo.
Serikali inatoa onyo kwa wale wote wanaosambaza picha isiyo rasmi pamoja na Serikali kusitisha matumizi ya picha hiyo na wale wote wanaotengeneza picha ukubwa usio rasmi, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"Kwani ni Idara ya Habari MAELEZO pekee ndiyo yenye Hakimiliki ya picha hiyo" alifafanua Bw. Hokororo.
"Kwani ni Idara ya Habari MAELEZO pekee ndiyo yenye Hakimiliki ya picha hiyo" alifafanua Bw. Hokororo.
Tunampongeza Mheshimiwa Rais Magufuli kwa kuanza "hapa kazi tu" vizuri sana sana kwa kusitisha matumizi ya fedha za serikali katika hafla na vitu vingine bila sababu za kimsingi, sasa tunauliza: kwa nini amekubali kulazimisha wananchi waingie gharama ya Tshs 15,000/= kununua picha yake?? Gharama hizo siyo bila sababu?
ReplyDeleteHapo anamuumiza mwananchi. Tshs 15,000/= ni hela nyingi sana, hata kwenye mwaka 2016. Halafu kutundika picha ya Rais kwenye maduka au ofisi binafsi haitakiwi kuwa lazima,tunaishi katika karne tofauti na ile ya zamani. Tumeshamkubali na kumpokea kama Rais wetu, basi kazi ziendelee...
Tunamtakia afya njema, maisha marefu na shughuli njema...
Nafikiri mimi kwa mtu anayeipenda Tanzania na kujivunia utanzania wetu Picha ya Rais ni muhimu kuwa nayo, hii inaonyesha mapenzi aliyonayo huyu baba kwa nchi yetu. Mungu ambariki Magufuli popote aendapo tupo.
Delete