Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kata ya Kanyelele jimboni humo kabla ya kuanza mkutano wake na wananchi hao uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mwakalima. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele ambapo kimeharibika. Hata hivyo, aliwataka wananchi hao waweke utamaduni wa kuchangia maendeleo ya vijiji vyao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akimuuliza swali Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kulia) wakati Mbunge huyo alipokuwa akikiangalia choo cha Shule ya Sekondari Kanyelele jimboni humo kilichobomoka. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akiwa na Diwani wa Kata ya Kanyelele, Paschal Kilangi (kushoto) pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kanyelele, Kudehwa Gapi (wapili kulia) wakiwa wanaikagua shule hiyo ambayo choo chake kilikuwa kimebomoka kwa kudidimia chini ya ardhi. Waziri Kitwanga alichangia shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho na kuwaomba wananchi wa kata hiyo waanze kuchanga kwa kasi ili choo hicho kiweze kutengenezwa kwa haraka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...