Mkurugenzi Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga,
kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja
vinavyotolewa na taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo,
Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services
inayojihusisha na mikopo, imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja
katika maeneo ya Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa
ni mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti kuungwa
mkono Watanzania wengi.
Kuzinduliwa kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa
na Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya
Temeke, Martha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania,
hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku, jambo
linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia wananchi wake kupata
maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga, aliyesimama akizungumza katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore, Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra Moore.
Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na njia rahisi kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wote kuchangamkia fursa ya upatikanaji wa viwanja hivyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...