Na Bakari Issa Madjeshi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limekataa rufaa ya Rais wa Shirikisho hilo ambaye anatoka madarakani, Sepp Blatter na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Ulaya (UEFA) aliyesimamishwa kazi, Michael Platini.
Kamati ya Rufaa ya FIFA imekataa rufaa ya Marais hao lakini imewapunguzia adhabu ya kujihusisha na masuala ya soka kutoka miaka nane hadi miaka sita.
Wote walipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha Paundi Milioni 1.3 sawa na Dola Milioni 2 ambazo Blatter alimlipa Platini kwa kile walichokiita kazi maalum.
Blatter na Platini walikataa kufanya hivyo na kusema kuwa wanakwenda katika Mahakama ya Rufaa (CAS) kukata rufaa.
Pia wamesema makubaliano ya malipo ya mwaka 1998 yalikuwa yakiungwana kwa kazi iliyofanywa na Mfaransa huyo wakati alipokuwa mshauri wa ufundi wa Blatter.
Hata hivyo,Blatter katika maelezo yake alieleza kuwa “sijakubaliana na Kamati ya Rufaa ya FIFA”.
Naye,Platini alisema kuwa “ni udharirishaji na aibu kwa maamuzi hayo ya kisiasa”.
Uchaguzi wa kumtafuta mbadala wa Blatter utafanyika siku ya Ijumaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...