1.LESENI HUTOLEWA
KWA NAMNA MBILI.
Unapohitaji
leseni ya kutafuta madini unapaswa
kujua kuwa leseni
hizi hutafutwa kwa
namna mbili tofauti. Kwanza kwa
maombi maalum na
pili kupitia zabuni. Sheria mpya
ya madini sheria
namba 14 ya
2010 ndiyo kiini cha
makala haya.
2.LESENI KWA
MAOMBI MAALUM.
Kwa maombi maalum
ni hatua ya
kawaida ya kuomba
kama ambavyo unaweza kuomba
kazi au tenda
yoyote ambayo haijatangazwa
na serikali. Hatua hii
huja baada ya
mjasiriamali kuliona eneo
la madini na
kuamini kuwa anaweza
kuwa sehemu ya
biashara ya eneo
hilo.
Maombi hufanywa katika
fomu maalum ambazo
hupatikana kwa kamishna
wa madini. Makamishna
wa madini hupatikana
hata wilayani au
mikoani hivyo inategemea
ni sehemu ipi unataka
kutafuta hayo madini.
Kubwa ni
kuwa utatakiwa kutumia
wilaya au mkoa
husika katika kupata
fomu hiyo kwa
ajili ya kutuma
hayo maombi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...