MWENYEKITI
wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo amesema anaguswa na kazi nzuri ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.
Paul Makonda katika ujenzi wa shule za sekondari za kata.
Bulembo
ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM alisema kutokana na jitihada hizo
ameona haja ya kumtia moyo DC Makonda kwa kuchangia ujenzi wa shule hizo saba
unaoendelea.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi saruji mifuko 500 Bulembo alimtaka
Makonda kuendelea kupigania utekelezaji wa Ilani bila kujali itikadi za vyama
katika kuleta maendeleo ya wilaya hiyo.
Alisema
Jumuiya ya wazazi kazi yake kubwa ni ulezi hivyo mafanikio yatakayopatikana
kutokana na wanafunzi zaidi ya 3183 waliokosa shule katika wilaya hiyo kuweza
kuendelea na masomo ni ya kujivunia.
Aliwataka
watendaji wa Manispaa hiyo kuhakikisha malengo ya ujenzi huo yanatimia ili
kuokoa watoto ambao wangeathirika kutokana na kukosa elimu.
Makonda aliwapongeza wote
wanaojitokeza katika kumuunga mkono katika ujenzi wa shule hizo na kusema jana
amepokea mifuko 1640 ya saruji.
Alisema
saruji hiyo ni mifuko 500 kutoka kwa Bulembo, 500 kutoka kwa Askofu Mkuu
mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex
Malasusa na mifuko 640 kutoka Kampuni ya The Duma Group.
Aliwahakikishia
wadau hao wa elimu kuwa atasimamia ipasavyo ujenzi wa shule hizo ili kupunguza
wimbi la watoto wasio na elimu Kinondoni ambao ndio chimbuko la vijana
wanaotumia dawa za kulevya,biashara ya ngono,vibaka,mimba za utotoni na
wahalifu wengine.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya The Duma Group, Areeq Amran Mohamed alisema lengo la kusaidia
saruji hiyo ni kuungana na serikali katika kutekeleza sera ya kuinua elimu
wilaya ya Kinondoni.
Akiongea baada ya kupokea misaada hiyo, DC Makonda alisema:
"Napenda kumshukuru sana Baba Askofu Malasusa kwa kunichangia mifuko 500 ya cement kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa.
"Pia namshukuru sana Mhe Abdallah Bulembo Mwenyekiti wa WAZAZI CCM Taifa kwa support ya mifuko 500 ya cement na mwisho, si kwa Umuhimu, bali kwa upande ni kampuni ya The Duma Group kwa mifuko 640 ya cement.
"Naowaombea kwa Mungu awape maradufu kwani kitendo hiki ni kitendo cha kiungwana. Mmetuvisha nguo wanaKinondoni. Nawe mtanzania mwenzangu kama unamchango wowote bado nakukaribisha.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda akipokea mifuko 640 ya cement kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Duma Group, Bw. Areeq Amran Mohamed
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda akitoa shukurani kwa Mhe Abdallah Bulembo mwenyekiti wa wazazi ccm Taifa kwa mchango wake wa mifuko 500 ya Cement.
KILA LA KHERI MAKONDA,UNAFANYA KAZI SAFI KABISA INAONEKANA ACHANA NA WANAOKUSEMA KWA UBAYA LAKINI KAZI YAKO INAONEKANA
ReplyDelete