
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira
akila kiapo cha kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na
Magereza mbele ya Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto)
jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi
kwa askari Polisi na Magereza. Katikati ni Msajili wa Mahakama Kuu,
Ilvin Mugeta.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni mara baada ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, Shabani Lila (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni kabla ya kumuapisha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza, katika tukio lililofanyika katika Mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari Polisi na Magereza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu, mara baada ya Jaji huyo kuwaapisha kuwa viongozi wa Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza katika tukio lililofanyika Mahakamani hapo, jijini Dar es Salaam leo. Injinia Masauni katika Tume hiyo amekuwa Makamu Mwenyekiti, na Meja Jenerali Rwegasira amekuwa Katibu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...