Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akiongea wakati wa kikao na wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) alipowatembelea katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa TBA Arch.Elius Mwakalinga.
Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani (hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam, katika ziara ya kuzitambua tasisi zilizopo chini ya wizara yake.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akimsikiliza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Manase Ole Kujan katika ziara yake ya kuzitambua tasisi zilizo chini ya wizara yake kwa kuangalia majukumu yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI,
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (UJENZI).
NAIBU Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, amezitaka taasisi zilizo
chini ya Wizara yake kufanya kazi kwa uadilifu, bidii na kwa uharaka ili
kuendana na kasi ya madiliko ya Serikali ya awamu ya Tano.
Ameyasema hayo wakati
alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini ya Wizara yake ikiwemo Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA), Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Baraza la Taifa
la Ujenzi (NCC) kwa lengo la kupata
mafunzo ya kiutendaji katika taasisi hizo.
Aidha amezitaka
taasisi hizo kuongeza ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vya mapato
walivyonavyo na kamwe kutotegemea ruzuku kutoka Serikalini.
“Nataka ifikapo mwaka
wa fedha ujao makusanyo ya mapato yawe yameongezeka zaidi kuliko matumizi na
kamwe msikae kusubiri ruzuku kutoka Serikalini, kikubwa ni kubuni vyanzo
vyengine vya mapato ili kuweza kujiendesha”, alisema Naibu Waziri.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo amewataka watendaji hao
kufanya kazi kwa weledi na bila woga kwani Serikali haitamuonea huruma yeyote
anayekiuka kutekeleza wajibu wake.
“Nawaomba mfanye kazi
kwa morali kubwa ili kuweza kuisaidia jamii ambayo inahitaji huduma muhimu
kutoka Serikalini”, alifafanua Eng. Ngonyani.
Katika hatua nyingine Eng.
Ngonyani amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole kujan kutatua
changamoto walizonazo ili kuleta mabadiliko chanya katika taasisi hiyo.
“Una nafasi kubwa ya
kuleta mabadiliko hasa katika mfumo mzima wa ukatikatishaji tiketi eneo la
Magogoni ambalo limekuwa kero katika mfumo mzima wa ukusanyaji wa mapato”, alisisitiza
Naibu Waziri Ngonyani.
Sambamba na hilo Naibu
Waziri amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Arch. Elius Mwakalinga, kuandaa taarifa ambayo
itaonyesha idadi ya nyumba za Serikali wanazomiliki na ibainishe taarifa ya watumishi
wenye stahili ya kupangishwa kwenye nyumba hizo.
Kwa upande wake Kaimu
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Eng. Manase Ole Kujan amesema wakala huo umepanga
kuboresha miundombinu hasa katika usafiri wa majini na kuhakikisha inapunguza changamoto ya usafiri katika vivuko.
Naye Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi, Eng. Julius Mamilo amebainisha
changamoto walizonazo ikiwemo uhaba wa fedha hali inayosababisha Baraza hilo
kukwama katika kufanya kazi katika miradi yake ya maendeleo hususan katika
kufanya kazi za utafiti.
IMETOLEWA
NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA
MAWASILIANO (SEKTA YA UJENZI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...