NANI: Amadou Gallo Fall –Rais
na Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu – Africa
Allison Feaster - Mchezaji nyota na Mwandamizi wa WNBA
Paul Hinks –Mtendaji Mkuu
wa Symbion Power
NINI: Kuanza
rasmi kwa Ligi ya Mpira wa kikapu kwa vijana (Jr.NBA Basketball League) nchini
Tanzani
LINI: Saa
saba Mchana, Siku ya Jumamosi; Tarehe 27,2016
WAPI: Kituo cha Vijana cha Michezo Jakaya
M. Kikwete jijini Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Kikapu litazindua rasmi msimu
wa kwanza wa ligi ya mpira wa kikapu kwa vijana kwenye kituo cha vijana cha
Michezo cha JMK jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 27 Februari mwaka huu.
Sherehe hii ya ufunguzi ambayo itahudhuriwa na
Mchezaji Nyota na Mwandamizi wa WNBA aitwaye Allison Feaster itakuwa ni uzinduzi
rasmi wa ligi ya Mpira wa Kikapu ya Vijana wenye umri kati ya miaka 12 na 14.
Ligi hii itajumuisha shule kutoka maeneo ya karibu zipatazo thelathini (30)
kila shule ikiwakilisha moja wapo wa timu 30 zinazoshiriki Ligi ya Mpira wa
Kikapu ya Marekani.
Wanahabari
ambao watapenda kushiriki kwenye uzinduzi huu wanapaswa kutoa taarifa ( RSVP)
kwa adi.raval@jmkpark.org kabla ya
tarehe 25 Februari saa kumi na moja jioni. Kituo kinachoruhusiwa kushiriki
kinapaswa kuwa na hadhi stahiki.
Ligi ya mpira wa kikapu ya vijana (Jr. NBA League) Ni
ligi ya NBA ya kidunia inayoshirikisha mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana ;
wavulana kwa wasichana na inafundisha stadi za msingi za mchezo wa mpira wa
kikapu pamoja na maadili muhimu ya mpira wa kikapu kwa wachezaji wanaoanza.
Lengo likiwa ni kusaidia kukuza na kuboresha uzoefu wa Wachezaji, Makosha na
Wazazi
Kwa maelezo zaidi kuhusu kituo cha Michezo
cha Vijana
tafadhali tembelea www.jmkpark.org.
***
FURSA ZA MAHOJIANO NA UCHUKUAJI PIA ZINAPATIKANA***
* * *Hii ni sherehe ya watu maalum – kama
ilivyoainishwa hapo juu, Waandishi wahabari wanaohitaji kuudhuria WANAPASWA kutoa taarifa mapema (RSVP)
kwa adi.raval@jmkpark.org kabla ya kumi
na moja ya siku Alhamisi ya Tarehe 25 Februari 2016 ili waweze kupewa ruhusa
kabla ya sherehe. Tafadhali mtumie Adi barua pepe kama una swali lolote.
Kwa Mawasiliano zaidi:
Pawel Weszka, NBA, pweszka@nba.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...