Kamanda Liberatus Sabas, alipokuwa akifunga Kampeni za ABIRIA PAZA SAUTI, Jijini Arusha,

 Na Vero Ignatus wa Wazalendo 25 Blog, Arusha.
Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewataka watu wote wanaomiliki silaha kwa njia halali wafike kwenye kituo cha polisi kuhakiki silaha zao na kuzilipia kama inavyostahili na kwa kufuata utaratibu kama sheria inavyoagiza. 
 Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, na kufafanua kwamba kila mwaka huwa kila mwenye silaha anafika polisi na silaha yake na vitabu vyake kwa ajili ya kuihahiki na kuilipia kama inavyostahili. 
Pia inaangaliwa  kama zipo tuhuma zozote kutokana na matumizi ya silaha hiyo  itasimamishwa kwa ajili ya taratibu zingine na kunyang’anywa hadi hapo jeshi litakapojiridhisha kuwa silaha hiyo matumizi yake ni sahihi ama siyo sahihi 
 Kamanda Sabas amesema utaratibu huu huwa unaratibiwa na makao makuu ya jeshi la polisi kwa ajili ya kuhakiki silaha, ikiwa ni pamoja na kulipia mapato ya serikali ,amewataka watu wanaomiliki silaha wafuate masharti yake kama inavyotakiwa. Amesema sheria inambana kila mtu mara anapotenda kosa ,na kama mtu akiitumia ndivyo sivyo atanyang’anywa silaha kwa kutumia sheria iliyowekwa. 
Ameongeza kuwa wapo watu ambao wamewatishia silaha wenzao,na wengine kesi zao zipo tayari na zingine zimefutiwa umiliki kwa mujibu wa sheria.
Kamanda huyo amesema kimsingi kabla mtu hajakabidhiwa silaha ili amiliki, yapo masharti ya kufuata na yapo kwenye kitabu kile cha leseni anachopewa wakati wa umiliki, na kwamba akienda kinyume na  hayo masharti huna sifa ya kumiliki silaha. 
 Kamanda Sabas ametoa anagalizo kwa wamiliki wa silaha na kusema kuwu silaha ya moto siyo kama panga,silaha hiyo ukiifanyia kosa mara moja yaweza kuua mtu au watu hivyo amewataka kuwa makini sana katika ufuatiliaji wa umiliki, pamoja na namna zinavyotunzwa,amesema jeshi la polisi lipo makini kufuatilia kwa ukaribu wakithibitisha silaha haitunzwi kama inavyostahili utanyang’anywa.aidha amesema kwa wazee amabao umri wao umeenda nab ado wanamiliki silaha huwa wanaichukua na kuihifadhi . 
Amehitimisha kwa kusema kuwa kila , mtu anayetaka kumiliki silaha, lazima kwanza akapitia kwenye kamati za ulinzi na usalama kuanzia kwenye kata, Wilaya, na Mkoa ambako wanamuidhinisha kuwa na silaha afuate masharti na kuitunza silaha isije ikaangukia kwenye mikono ya wahalifu wakaitumia isivyo halali sheria itafuata mkondo wake.
Silaha huwa zinatakiwa kulipiwa kila mwaka kuanzia mwezi julai hadi septemba ukichelewa kulipia unapigwa penati kwa mujibu wa sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...