Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ameitumia salamu za Rambirambi familia ya Mzee Dellan Tarmo kufuatia kifo cha  kijana wao mpendwa Jovitha Dellan kilichotokea kwa ajali ya gari mkoani Arusha juzi tarehe 31.1.2016.

“Pokea rambirambi zangu za dhati, sote kwa pamoja tumepoteza kijana  mchapakazi, hodari na aliyependa kushirikiana na wenzake katika kazi zake, hakika tutamkumbuka siku zote” Katibu Mkuu amesema.

Katibu Mkuu, Pia amemtumia salamu za pole kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu(KBF) na Wafanyakazi wote wa Bodi ya  Filamu Tanzania.
“Nimepokea taarifa za kifo cha Jovitha Dellan kwa huzuni kubwa, najua machungu na maumivu mliyonayo kwa kuondokewa na kiungo muhimu katika utendaji wenu, poleni sana,  niko nanyi katika msiba huu mzito kwenu”, amesema Katibu Mkuu huyo.

Katibu Mkuu amesema pamoja na kwamba kifo hakiepukiki, bado ni kitu ambacho kinashtua, kuhuzunisha na kuleta unyonge mkubwa kwa wafiwa katika jamii.
 “Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu kumuombea kijana wetu Jovitha Dellan ili mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema ya Milele” Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape uvumilivu na subira katika kipindi hiki”.
“Niko nanyi katika kipindi hiki kigumu kwa hali na mali, nawaomba msijisikie wapweke” Katibu Mkuu amesema na kuwatakia utulivu na amani katika kipindi hiki cha msiba mkubwa kwa familia.

Marehemu Jovitha Dellan  amefariki juzi tarehe 31 Januari, 2016 mkoani Arusha ambapo alikuwa njiani kurejea kazini jijini Dar es salaam.
          Marehemu Jovitha Dellan anatarajiwa kuzikwa wiki hii mkoani Manyara.

          Jovitha Dellan alikuwa ni Afisa Utamaduni aliyekuwa akifanya kazi katika Bodi ya Filamu Tanzania iliyopo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu 
Jovitha Dellan mahali Pema Peponi - Amina.

Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO)
DSM.
2 Februari, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...